VATICAN CITY - Papa Francis, siku ya Jumatano 24/1/2018 ameshambulia habari za uongo na kusema ni jambo la kishetani kabisa. Amewataka wanahabari na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuachana na jambo hilo ambalo huweza kuchochea migawanyo ya kisiasa na kiuchumi pia ili kuhudumia matakwa binafsi ya baadhi ya watu.
Papa Francis ameyasema hayo ambayo pia yaliandikwa katika Makala yake iliyochapishwa miezi kadhaa baada ya mdahalo wa namna taarifa za uongo zilivyo athiri kampeni za uchaguzi wa Uraisi wa Donald Trump huko marekani 2016. Amehusianisha pia habari za uongo na mbinu ambayo Shetani aliitumia katika bustani ya Edeni kumdanganya Eva na Adam.
Source : ABS-CBN Corporation
No comments:
Post a Comment