KUSHUGHULIKA NA
MTAZAMO
4th
February 2018
By Pastor
Sam Gripper
MAANA YA
MTAZAMO
Ni mwenendo, tabia au muitikio wa mtu juu ya
jambo flani, ni namna jambo linavyotazamwa na kuonwa kiujumla. Sote tunaweza
kufanana katika namna ya maumbile, lugha, asili na mambo mengine kama hayo,
lakini sio kweli kwamba sote tunaweza kuwa na mtazamo sawa.
Msingi wa tofauti zetu huanzia katika point
hii ndogo na isiyoonekana. Mawazo yako, muitikio wako juu ya jambo fulani,
namna unavyofanya maamuzi na kupima mambo mbalimbali, ndiyo hasa hutafsiri wewe
ni nani, lakini zaidi hukutofautisha na wengine.
KWELI KUU 3 KUHUSU MTAZAMO NA MUITIKIO WAKO JUU YA JAMBO
Ukweli wa
kwanza,
vitu vingi vinavyokatishaga au kuzuia safari zetu huwa sio matatizo wala haviji
kama matatizo, lakini shauku yetu (nguvu inayotusukuma juu ya mambo
tunayotarajia), mtazamo na muitikio wetu juu ya mambo kama hayo, ndiyo hasa
huvifanya vitu hivyo vionekane kama tatizo au vizuizi vya sisi kuendelea.
“Bwana akamwambia Musa, mbona unanililia mimi? Waambie wana wa
Israel waendelee mbele. Nawe inua fimbo yako, ukanyoshe mkono wako juu ya
bahari, na kuigawanya, nao wana wa Israeli watapita kati ya bahari katika nchi
kavu”
KUTOKA
14:15-16
Jambo ninalotaka tulitazame hapa ili pia
linisaidie katika kuielezea point yangu ya kwanza ni kwamba, asilimia kubwa ya mambo
yanayotuzuia sio matatizo na hayaji kwetu kama matatizo. Historia zetu, shauku
zetu, muitikio na mitazamo yetu ndiyo hasa hufanya mambo haya yawe matatizo.
Mwanzo 1:31, inaposema Mungu alikiona kuwa
kila alichokiumba ni kamilifu na chema, kati ya hivyo ilikuwemo pia Bahari ya
Sham. Na alipokuwa anaiumba, hakuwa analiumba tatizo wala zuio la Wana wa
Israeli kutoka Misri. Hivyo bahari haikuwa tatizo. Nataka kuamini kuwa
zilikuwepo shughuli nyingi tuu za kiuchumi zilizokuwa zinategemea uwepo wa
bahari hii na wafanyaji wa shughuli hizo, waliichukulia na kuitazama bahari
kama fursa kwao na sio zuio au tatizo.
Lakini historia ya wana wa Israel, shauku
waliyokuwa nayo ya kutoka mikononi mwa watesi wao, mitazamo na muitiko wao
walipokutana na bahari ile ndiyo hasa vilifanya ionekane kama tatizo na zuio la
safari yao, lakini katika namna halisi ya uumbaji, bahari ya Sham haikuwa
tatizo.
Na ndio maana mara baada ya Mungu kuwapa
“mtazamo wake” kwamba hata bahari inaweza kuwa njia na kuwavusha, hakuiacha
iendelee kuwa njia kwa wengine kwasababu hakuiumba ili iwe njia ila iwe bahari,
na akairudisha kama ilivyokuwa kwasababu ilikuwa ni zuio kwa wana wa Israel
tuu, lakini kwa wengine ilikuwa ni fursa. Hivyo kama Mungu angeiacha iendelee
kuwa njia, angekuwa ameziharibu fursa za watu wengine waliokuwa wakiitegemea
bahari ile ili kuendesha maisha yao.
Nataka kuzungumza nini hapa? Ni hivi, yapo
baadhi ya mambo ambayo kimsingi yaliumbwa kuwepo na yalitakiwa yawepo katika
maisha ya kila siku. Lakini shauku yetu ya kufika mahali, mitazamo na miitikio
juu ya mambo kama hayo, vinaweza kutuambia kuwa mambo hayo ni matatizo na
vizuizi vya sisi kuendelea. Katika point kama hii, hatuwezi kuyavuka mambo kama
hayo, pasipokujua mtazamo wa Mungu juu ya mambo hayo.
Wana wa Israel walipokutana na bahari,
hawakuwa na haja ya kumwomba Mungu aikaushe. Na maandiko yanaeleza wazi kuwa
hawakuwa na jambo la kufanya zaidi ya kumlaumu Musa. Mtazamo na muitikio wao
kwa uwepo wa bahari ile ulikuwa ni kuiona ile bahari ni tatizo na zuio. Jambo
kuu ambalo lilikuwa ni ukombozi kwao, lilikuwa ni kumsikiliza Mungu ana mtazamo
gani juu ya hali iliyokuwa mbele yao ambayo kimsingi haikuwa tatizo kwa Mungu.
Hivyo, tunahitaji kuwa na akili, ufahamu na
nia (mind) ya Kristo na mtazamo wake, tunapodeal na mitazamo yetu katika
kutatua na mambo yanayotuzunguka.
“Basi mwanadamu wa tabia ya siri, hayapokei mambo ya Roho wa Mungu
maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwakuwa yatambulikana kwa
jinsi ya rohoni. Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na
mtu. Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo
nia ya Kristo.”
1WAKORINTHO
2:14-16
Nia ya Kristo ndani yetu, ndiyo hasa
hushughulika na kuibadili mitazamo yetu. Sio mara zote mambo tunayokutana nayo
huwa kama matatizo, lakini mitazamo yetu huweza kufanya yaonekane kama ni matatizo.
Tunapokuwa na nia au ufahamu wa Kristo tunayatazma kama yeye ayatazamavyo.
Ukweli wa
pili, Kikawaida
mtazamo wa mtu huwa unaathiriwa sana na position aliopo. Kama utautazama Mlima
Kilimanjaro ana kwa ana, ni mlima mrefu ambao kwa namna yoyote huwezi kuuvuka
na kwenda upande mwingine. Lakini ukiutazama mlima huo huo kutokea juu,
hutauona kwa urefu ambao uliuona ulipokuwa unautazama ana kwa ana. Utauona ni
kama kidoti fulani tuu. Hii ni kwasababu, position yako imebadilika.
Kulingana na eneo/ mahali ulipo, kila
unachokiona kina nafasi kubwa sana ya kukutafsiri na kuyatafsiri maisha yako
kwa vile ulivyokiona, kulingana na mahali ulipo. Nuru na giza haviwezi
kukubaliana juu ya kitu kimoja, na ndio maana maandiko yanatuambia kuwa hapana
urafiki kati ya mtu wa giza na mtu wa nuru kwasababu ya utofauti wa position
walizopo.
“Niyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu. Lakini
Mungu kwakuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata
wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na
Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. Akatufufua pamoja naye, akatuketisha
pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu.”
EFESO
2:1,4-6
Mstari wa kwanza wa kitabu cha Waefeso sura
ya 2, unaanza kueleza juu ya position tulizokuwepo katika maisha yetu ya kale. Tulikuwa
wafu kwasababu ya makosa na dhambi zetu. Kwa jinsi hii, ni wazi kwamba kuna
namna mitazamo yetu iliathiriwa na position tulizokuwepo. Tulideal na mambo
yanayotuzunguka kulingana na wapi tulipo. Lakini ashukuriwe Mungu ambaye kama
namna ya kuanza kudeal na mitazamo yetu, alianza kubadilisha position tuliopo.
Mstari wa 4, unaanza kuelezea kuwa
alituhuisha pamoja na Kristo, na mistari iliyobaki inasema, akatuketisha pamoja
na Kristo katika ulimwengu war oho. Hivyo ni wazi kuwa, hatutakuwa tukiyaangalia
mambo na kudeal nayo kama tulivyokuwa tukideal nayo tulipokuwa wafu kwasababu
ya dhambi na makosa yetu, lakini tutayatazama na kudeal nayo kama Kristo
anavyoyatazama maana tumeketishwa pamoja naye.
Ukweli wa
tatu, mtazamo
wako haumuathiri mtu mwingine yeyote isipokuwa wewe mwenyewe. Na hili ndilo
jambo baya na hatari sana kuhusu mtazamo wa mtu. Wakati umeruhusu jambo flani
lionekane ni tatiz kwako, jambo hilohilo kwa mwingine linaweza kuwa ni fursa
ambayo itampelekea kufanya mageuzi makubwa ya hali yake husika.
Watu wote waliofanya ugunduzi mkubwa wa
viombo vya usafiri, njia za mawasiliano na mambo kama hayo, hawakuruhusu kuona
mambo yanayowazunguka kama matatizo, badala yake waliyaona kama fursa
zinazowapelekea katika ugunduzi wao mkubwa. Na kwa upande mwingine, watu wote
waliokubali kukata tamaa, ni watu ambao hawakutaka kubadlisha mitazamo yao juu
ya mambo wanayokutana nayo.
Siri ya ukuu wa mtu inaanza katika namna
anavyotumia mtazamo wake katika kushughulika na mambo yanayomzunguka. Mtazamo
hasi, hauwezi kuona jema hata katikati ya mema, lakini mtazamo chanya huweza
kuhesabu mema hata katikati ya mabaya. Sio matatizo yanayotukwamisha, lakini ni
mitazamo yetu juu ya matatizo hutukwamisha. Badili mtazamo ili ubadili maisha.
© Pastor Sam
Gripper
TAG PENUEL
LUHANGA
#2018betransformed
TOTAL
TRANSFORMATION
No comments:
Post a Comment